F Msanii Mbosso aibua jipya kwenye muziki wake | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Msanii Mbosso aibua jipya kwenye muziki wake


Msanii wa Bongo Fleva, Mbosso ameeleza sababu ya kujipachika jina la Mr. Roamntic kwenye muziki wake.

Muimbaji huyo kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times FM amesema alivyofanya pindi alipokuwa akienda kwenye show nchini Kenya.

"Nilipata mwaliko kule Kenya, sasa ilibidi niposti ile, sasa si unajua watu wa Kenya wanapenda Kiingereza zaidi, na mimi Kiingereza kinanichanganya sana, ikabidi nimpe meneja wangu Sandra aniandikie caption," amesema Mbosso.

Ameendelea kwa kusema, 'Nikamtumia kil a kitu, basi alivyorudisha nikaona Mr. Romantic, nikashangaa nikamuuliza kwanini umeweka hii, akasema inanifaa nijaribu, nikaenda nayo watu wakaipokea vizuri, basi nikaenda nalo hivo Mr. Roamntic,'.