Serikali ya Tanzania kupitia wawakilishi wake nchini Canada wamekabidhiwa ndege mpya nyingine mpya Airbus.
Hiiinakuwa ni ndege ya pili aina ya Airbus kukabidhiwa ambayo tayari imepewa jina la Ngorongoro Hapa Kazi Tu. Ndege hiyo inatarajiwa kuwasili nchini mapema mwaka huu.
Utakumbuka serikali katika jitihada za kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imepanga kununua ndege saba, hadi sasa ndege tatu ndogo aina ya Bombardier Q400 zimeshawasili, pamoja na Boeing 787-8 Dreamliner na Airbus 220-300.