Muonekano wa jengo la Wizara ya TAMISEMI mara litakapokamilika. Jengo hili linajengwa katika Mji wa Serikali jijini Dodoma, ambapo ujenzi wake unagharimu Tsh.Bilioni 1. Kitengo cha Ujenzi cha Chuo Kikuu Mbeya ndio fundi ujenzi, chini ya Wakala wa Majengo (TBA) kama mshauri.