F Wachezaji 20 wa Simba SC kuondoka leo kuifuata Al Ahly | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wachezaji 20 wa Simba SC kuondoka leo kuifuata Al Ahly


Kikosi cha wachezaji 20 wa Simba SC wanaondoka leo nchini majira ya jioni kuelekea Misri kwa
ajili ya kucheza mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Simba SC itaondoka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia na kisha kuelekea Mjini Alexandria, Misri ambapo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa February 2 mwaka huu.

Utakumbuka kuwa Simba SC itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi AS Vita ya DR Congo kwa kulala kwa goli 5-0.