F Wachezaji wapya Simba SC waanza kumpagawisha kocha | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wachezaji wapya Simba SC waanza kumpagawisha kocha


Hivi karibuni Wekundu wa Msimbazi walileta wachezaji wa kigeni kwa ajili ya majaribio. Hadi
sasa inaelezwa kuwa beki Lamine Moro kutoka Ghana amemvutia Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems.

Kocha huyo amesema amefurahishwa na kiwango cha beki huyo kwa dakika alizomuona akiwa uwanjani akicheza dhidi ya AFC kwenye michuano ya SportPesa.

“Nimeangalia upigaji wake wa pasi, ukokotaji wake mpira na ukabaji katika kuokoa na ku­zuia mashambulizi yupo vizuri Moro, lakini ninahi­taji muda wa kumuangalia vizuri," amesema Aussems.

Wachezaji hao waliotua nchini kwa ajili ya majaribi kwenye timu hiyo ni Hunlede Abel kutoka
Togo, Sadney Urikhob kutoka Namibia na Lamine Moro kutoka Ghana.