Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Asiah Abdallah amezindua zoezi la Upandaji Miti ya Matunda aina ya Parachichi katika maeneo ya Taasisi za serikali zoezi lililofanyika katika Shule ya Msingi Ng'ang'ange.
Akizindua zoezi hilo mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kuchangamkia fursa kwa kupanda miti ya matunda kutokana na uwekezaji wa viwanda vya kusindika matunda unaotarajia kufanyika siku za Usoni.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kufanya hivyo kutawakomboa kimaisha kwa muda Mfupi badala ya kuendelea kupanda miti ambayo faida yake inapatikana baada ya miaka 15.