Jinsi unavyo zidi kutumia pasi hiyo ndivyo uchafu chini ya pasi unavyo zidi kujaa na kufanya upigaji pasi kuwa mgumu. Thank god tatizo hilo si tatitizo tena kwani nina njia moja rahisi sana wala haigharimu hata senti tano.
Jinsi ya kusafaisha
Chukua kipande kimoja cha mkaa
Jinsi ya Kufanya.
Chukuwa kipande cha mkaa, ukubwa utachangia uharaka kwani utasafisha eneo kubwa na kufanya kazi hiyo na kumalizika haraka. Ili kufanikiwa haraka lazima mkaa huo uwe ulisha tumika jikoni na kupoa (Uliozimika)siyo ule uliozimwa kwa maji. Ili kuzima mkaa vizuri itabidi uufunike na chombo kukibwa kama sufuria nk kwani mkaa ukikosa oksijeni huzimika taratibu.
Washa pasi yako kama niya umeme, kama niya mkaa basi ipashe moto iwe na joto fulani hivi. Kumbuka jinsi pasi inavyokuwa na umoto rahisi inakuwa kuisafisha! Chukuwa kipande hicho cha mkaa sugua eneo la pasi lililozingirwa na uchafu (mgando mweusi) . Endelea kusugua hadi utakapo ridhika kwamba ni kweli imesafishika.