F Kikosi cha Yanga SC chawasili Mwanza | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kikosi cha Yanga SC chawasili Mwanza


Kikosi cha Yanga SC, kimewasili Jijini Mwanza Leo tayari kwa  mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Alliance FC.

Kuelekea katika mchezo huo Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amesema ligi ina ushindani na wapo tayari kupambana kwa ajili ya kusaka alama tatu.

Yanga itacheza na Alliance Machi 2 ambayo itakuwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, mechi hiyo inaenda kupigwa huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mechi yake iliyopita dhidi ya Mbao FC, Ikumbukwe Yanga ipo kileleni kwa alama 61 nyuma ya Azam iliyo na 50 na Simba ikiwa na 48.