F Manara amvisha jezi ya Simba DC Muro aliyewahi kuwa Msemaji wa Yanga | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Manara amvisha jezi ya Simba DC Muro aliyewahi kuwa Msemaji wa Yanga



Kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid dakika chache kabla ya mchezo, Msemaji wa Simba Haji Manara amemvisha jezi ya Simba Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye shabiki na aliwahi kuwa Msemaji wa Yanga.

Julai 14 mwaka 2017 klabu ya Yanga kupitia kwa aliyekuwa katibu wake Mkuu kwa wakati huo, Charles Boniface Mkwasa ilimtambulisha, Jerry Muro kuwa msemaji wa timu hiyo na kutikisa sana katika nyanja ya kimichezo hasa kufuatia ushindani wake dhidi ya Haji Manara ambaye anatokea upande wa hasimu wao Simba SC.

Wiki iliyopita Yanga imejikuta ikipoteza mchezo wake dhidi ya Simba baada ya kufungwa bao 1 – 0 kwenye mechi ya ligi kuu soka Tanzania Bara.