F Msanii maarufu nchini Kenya afariki dunia | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Msanii maarufu nchini Kenya afariki dunia


Msanii wa Muziki wa Hip hop nchini Kenya Chris Kantai mwenye umri wa miaka 42 amefariki dunia jana katika Hospitali moja mjini Nairobi.

Vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa Msanii huyo alilazwa tangu Jumatatu wiki hii na kupokea matibabu kwa muda mfupi.

Gazeti moja limemnukuu mwakilishi wa familia ya msanii huyo Bi Wanjiku Thuku, aliyesema kwamba alifariki kutokana na matatizo ya kupumua.