Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amezindua maabara ya uchunguzi na tiba ya moyo (Cathlab ) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.
Hospitali ya Benjamin Mkapa sasa inakuwa hospitali ya pili kuwa na maabara hiyo ambayo inatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa nyanda za kati na kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu Dar Es Salaam pamoja na nje ya nchi.