F Tuliposikia ishu ya Nandy na Billnas mioyo ilisimama - Baba Nandy | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Tuliposikia ishu ya Nandy na Billnas mioyo ilisimama - Baba Nandy


Baba mzazi wa msanii, Nandy, Charles Mfinanga ameeleza kitu kilichowapa shida kwa mtoto wa Nandy tangu aanze muziki.

Mzee Mfinanga amesema kuwa alipoona video ya Nandy na Billnas ya faragha mioyo yao ilisimama kwa muda kwasababu kwenye maisha yao hawakutegemea kama wanaweza kukutana kitu cha namna hiyo.

"Ishu yake na Billnas ile ilitufanya mioyo ilisimama muda fulani, kwasababu kwenye maisha yetu hatukutegemea anaweza kupata kitu cha namna hiyo, tumeshangaa simu nyingi zinapigwa angalieni huko kuna nini watu walikuwa wanashutumu kama vile ni mimi nimefanya kile kitu ndugu jamaa na marafiki ikawa ni tabu kabisa," Mzee Mfinanga ameiambia The PlayList ya Times FM.

Mwaka jana video ya Nandy na Billnas ilienea mitandaoni wakiwa faragha ishu ambayo watu wengi hawakupendezewa nayo.