Wachezaji wa Yanga SC, Feisal Salum Feitoto na beki Gadiel Michael watakosa mechi ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC, itakayochezwa Februari 20 mwaka huu katika Viwanja vya CCM Kirumba Mwanza.
Wawili hao wataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano hivyo kwa mujibu wa sheria za soka itawabidi kutohusika kwenye mechi hiyo.
Tayari kikosi cha Yanga kimeshafika jijini Mwanza na jioni ya leo kitaanza amzoezi kuelekea kipute na Mbao Jumatano ya wiki hii.
Yanga itakuwa inaenda kucheza mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 1-0 jijini Dar.