F ATCL yakanusha kuuza ndege ya Airbus A220-300 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

ATCL yakanusha kuuza ndege ya Airbus A220-300


Shirika la Ndege nchini, ATCL, limekanusha uvumi kuwa moja ya ndege zinazomilikiwa na Shirika hilo aina ya Airbus iko mbioni kuuzwa nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa za kumbukumbu za anga kupitia mtandao wa Flightradar24, Ndege namba 5H-TCH aina ya Airbus, A220-300, iliondoka Dar es Salaam majira ya 9.17 mchana kuelekea Nairobi Kenya, na majira ya saa 12 jioni iliruka kutokea Uwanja wa Jomo Kenyatta kisha kutua katika Uwanja huohuo muda wa saa moja jioni.


Aidha ndege hiyo iliondoka Nairobi saa nne usiku na kutua Dar es Salaam saa 5 na dakika 43 usiku.

Taarifa za ndani kutoka ATCL, zinasema Ndege hiyo ilikodiwa kwenda kufanya maonyesho ya ndege nchini Kenya, kisha ilirejea hapa nchini.