F Baada ya Transfoma kulipuka Mlandizi, Tanesco yaomba radhi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Baada ya Transfoma kulipuka Mlandizi, Tanesco yaomba radhi



Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema baadhi ya maeneo ya Mlandizi mkoani Pwani yatakosa umeme kutokana na transfoma katika kituo cha kupoza umeme kulipuka.



TANESCO kupitia ukurasa wao wa Twitter wameomba radhi kwa baadhi ya maneneo kukosa Umeme kulipuka huku ikielezwa kuwa kuungua kwa Transfoma kumeanza leo saa 1 asubuhi.

"Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Mlandizi na Bagamoyo kuwa leo Machi 30, 2019 majira ya Saa 1:50 asubuhi, Transfoma katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mlandizi imelipuka na kusababisha Mlandizi na baadhi ya maeneo ya Bagamoyo kukosa,"

"Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi ili umeme urejee katika hali yake. Aidha, uchunguzi unafanyika kubaini chanzo cha mlipuko huo.

"Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza."