Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo Oscar Mukasa amesema suala la upatikanaji wa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ni jambo la kitaifa na kamati yake inakakati wa kuhakikisha kwamba inaongeza nguvu kwenye mfuko wa Taifa wa Ukimwi na kuweza kujitegea kama nchi kuhusu masuala ya ya Ukimwi.
“Tuna haja ya kujipanga wenyewe kuhakikisha kwamba tunajitegema wenyewe na ule utegemezi wa fedha za wadau za mapambano ya Ukimwi unaweza kupungua” amesema Mhe. Mukasa.