F Kesi ya viongozi 9 wa CHADEMA kusikilizwa siku mbili mfululizo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kesi ya viongozi 9 wa CHADEMA kusikilizwa siku mbili mfululizo


Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu,imepanga siku mbili mfululizo, kusikiliza ushahidi katika kesi ya kufanya mikusanyiko isiyohalali,inayowakabili viongozi tisa wa CHADEMA.

Washtakiwa katika kesi hiyo namba 112/2019 ni M/kiti wa Chadema Taifa,  Freeman Mbowe (Mb), Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji, wengine ni NKMB John Mnyika (Mb), NKMZ,  Salum Mwalim, Halima Mdee (Mb), John Heche (Mb), Ester Matiko (Mb), Ester Bulaya (Mb), Peter Msigwa (Mb).

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.