Wakazi wa Kigoma wametakiwa kuacha tabia ya kuharibu miundombinu ya barabara ili Makao makuu ya Mkoa yasiwe kama kijiji.
Hayo yamesemwa Leo na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga
round about ya Mwanga kwenye zoezi la uzinduzi wa picha ya sanamu ya samaki aina ya mgebuka kama utambulisho wa rasilimali kwa wageni kwa Mkoa wa Kigoma.
Maganga alisema baadhi ya wakazi Kigoma siyo waaminifu wamekuwa wakifanya uhalifu wa kuharibu miundombinu ya barabara iliyowekwa na serekali kwa gharama kubwa hali inayofanya mji kushindwa kuendelea na kuwa wa kisasa.
"Serikali yetu imekuwa ikitumia fedha nyingi kuboresha miundombinu ya barabara lakini kuna wahalifu wachache wamekuwa wakiharibu miundombinu hiyo,tulifunga za sora za barabarani zikaibiwa mji ukawa giza,yeyote atakayekamatwa anaharibu miundombinu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake."alisema Maganga
Maganga pia amewataka wakazi wa Kigoma kutunza mazingira kwa kuweka maeneo yao ya makazi na biashara kuwa safi,pia kuacha tabia ya kuacha mifugo inazagaa ovyo mitaani na barabarani.