Koffi Olomidé, ambae ni nyota wa muziki Afrika , amepatikana na hatia ya ubakaji wa mnenguaji wake alipokuwa miaka 15.
Amehukumiwa miaka miwili gerezani na mahakama ya Ufaransa akiwa hayupo, baada ya kukosa kufika mahakamani.
Uamuzi huo una maana kwamba nyota huyo wa Congo atakamatwa iwapo atatekeleza uhalifu mwingine, anasema mwandishi wa BBC Nadir Djennad.
Olomidé, mwenye umri wa miaka 62, aliagizwa alipe Euro 5,000 kwa madhara aliyomsababishia mnenguaje wake huyo wa zamani.
Mahakama ya Nanterre, nje ya mji mkuu Paris, pia ilimuagiza alipe faini ya kiwango sawa kwa kuwasaidia wanawake watatu wengine kuingia nchini Ufaransa kwa njia haramu.
Wakili wa Olomidé amepongeza uamuzi huo na kuutaja kuwa ushindi, akiwarifu waandishi habari kwamba uamuzi huo utachangia kuondolewa waranti wa kimataifa wa kumkamata.