F Matokeo ya mtihani wa darasa la Nne, la Sita na Kidato cha Pili kwa mwaka 2018 yatangazwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Matokeo ya mtihani wa darasa la Nne, la Sita na Kidato cha Pili kwa mwaka 2018 yatangazwa



Akitangaza matokeo hayo Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo anaeshughulikia Taaluma Madina Mjaka Mwinyi alisema jumla ya wanafunzi 88743 wamefaulu kati ya wanafunzi 116,029 waliosajiliwa kufanywa mitihani kwa darasa la Nne,sita na Kidato cha Pili ambapo ufaulu huo umeongezeka ukilinganisha na mwaka 2017.

Alisema wanafunzi 116,029 wamefaulu na kuendelea nagazi nyingine ambapo darasa la Nne  31,317 sawa na  asilimia 70.4 Darasa la 33,519 sawa na asilimia 96.3 na kidato cha Pili wanafunzi 23,907 wamefaulu sawa na asilimia 42.85.

Aliongeza kwa kutaja kutaja ufaulu wa masomo umeongezeka mwaka 2018 ulinganisha na mwaka 2017 ambapo somo la Sayansi limeongoza kuwa na ufaulu wa juu ya asilimia 90 likifuatiwa na somo la dini lenye asilimia 87.7.


“kwa masomo ya hisabati lipo chini ya ufaulu kwa Asilimia 60.7 ya masomo mengine” alibaiisha Katibu mkuu.

Kwa upande mwingine Bi Madina aliwataja wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kitaifa ni Mwanafunzi Anuary Ali Darasa la Nne kutoka skuli ya Madrasatuli Ahbab, mwanafunzi Daudi Makame kutoka Skuli ya Mwembe Makumbi Darasa la sita skuli ya mwembe makumbi na mwanafunzi Ally Suleiman Ali kutoka skuli ya madungu upande wa kidato cha pili.

“kwa upande wa skuli zilizofaya vizuri Skuli ya feza imeongoza mitihani ya Darasa la Nne,Skuli ya Trifonia Academy inameongoza upande wa darasa la sita na Skul ya Sekondari ya Lumumba inaongoza mitihani kwa kidato cha pili” alieleza.