Mchezaji wa klabu ya mpira ya yanga abdallah Shaibu amefungiwa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, kwa kosa la kitendo cha utovu wa nidhamu ambapo alimpiga kiwiko mchezaji wa timu pinzania ambapo amefungiwa michezo mitatu.
Vilevile mchezaji wa Alliance FC ya mwanza Juma nyanji ambapo alilalamikiwa kwenye kamati ya upinzani kwa kosa la utovu wa nidhamu na udhalilishaji kwa mchezaji wa yanga Gadiel Michael ambapo alikiri kosa na kuomba msamaha kitendo cha kumshika makalio mchezaji huyo, na kamati ya maadili ilimpa adhabu ya kumfungia michezo mitatu na faini ya millioni 2.