Mahitaji
Pumba ya mahindi sadolini 1.
Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
Dagaa sadolini 1.
Kilo moja ya soya.
Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.
Namna ya kuandaa
Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
Saga hadi zilainike.
Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
Anika kwenye jua la wastani.
Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.