F Njombe: Kesi ya Mauaji ya watoto watatu imeendelea | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Njombe: Kesi ya Mauaji ya watoto watatu imeendelea


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Njombe imeahirisha kesi ya mauaji ya watoto watatu wa familia moja inayowakabili watuhumiwa watatu Mkoani humo hadi April 9 mwaka huu.

Kesi hiyo ambayo imesomwa na hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Njombe, Magdalena Mtandu imesogezwa mbele hadi muda uliopangwa kwa madai ya kwamba upelelezi wake haujakamilika ambapo mapema baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa katika Mahakama Kuu kujitetea juu ya tuhuma dhidi yake..

Watuhumiwa hao watatu wanatuhumiwa kwa makosa ya utekaji na mauaji  ya mtoto Gasper Nziku ,Giliard Nziku na Godwin Nziku ambao ni wa familia moja ambapo kwa mara ya kwanza watuhumiwa wote watatu ambao ni Jeol Nziku(35),Nasson Kaduma(39) na Alphonce Edward(51) walifikishwa mahakamani februari 12, 2019.

Katika hatua nyingine Mtuhumiwa Joel Nziku amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Njombe, James Mwanuchi kujibu shitaka linguine linalomkabili la kumteka mtoto Gaudence Kiyombo katika kijiji cha Ikando wilayani Njombe Mkoani Njombe ambapo hadi sasa mtoto huyo hajapatikana.

Watuhumiwa wote wamerejeshwa rumande hadi hapo tarehe ya kusikilizwa kesi hizo itakapowadia.