Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume amewasili mkoani Songwe akiwa ameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde kwa lengo la kuandaa na kukagua maandalizi ya mbio za mwenge ambazo kitaifa zinazinduliwa mkoani humo, tarehe 2, April mwaka huu.
Wakiwa mkoani humo wametembelea baadhi ya sehemu za vivutio kama kimondo cha Mbozi ambacho ni fahari ya mkoa huo.