Na. Clavery Christian, Bukoba
Afisa Masoko katika soko kuu la Bukoba mkoani Kagera, Yahaya Isheabakaki amesema kuwa Senene na Viazi Vikuu ni moja ya vyakula vinavyopendwa sana na watalii wanaokuja kutalii mkoani kagera kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini na dunia kwa ujumla.
Akizungumza na
Muungwana Blog katika ofisi za soko kuu la Bukoba, Isheabakaki amesema kuwa senene kimekuwa ni chakula ambacho kinapendwa sana na watalii wanaokuja hapa mkoani na likiwa ni zao linalopatikana kwa msimu na kwa uchache sana huku likitafutwa kwa kutumia utaalamu wa aina yake.
Isheabakaki amesema kuwa kwa upande wa zao la viazi vikuu ni zao linalopatikana kwa msimu pia na likiwa linalimwa baadhi ya maeneo ya mkoa kagera na kupendwa na watu wengi huku likisadikika kuwa chakula kitamu sana.
Aidha amesema kuwa ili kukuza kukuza uchumi wa mkulima katika mkoa wa kagera serikali inabidi iwawezeshe wakulima pembejeo za kilimo na kuwaomba maafisa ugani kujenga tabia ya kutembelea wakulima na kuwafundisha jinsi ya kulima kilimo cha kisasa ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda.
Afisa masoko katika Soko Kuu la Bukoba ameiomba idara ya mipango miji kutenga maeneo yenye ukubwa wakutosha pale wanapokuwa wanatenga viwanja kwa ajiri ya kujenga soko ili kuendana na wingi wa wafanyabiashara make watu wanaotaka kufanya biashara wanazidi kuongezeka kila kukicha na biashara zinazidi kukua na kuongezeka.