F Serikali yashauriwa kuongeza kima cha chini cha mshahara | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Serikali yashauriwa kuongeza kima cha chini cha mshahara


Na Enock Magali, Dodoma

Chama cha wafanyakazi wa Taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) kimeishauri serikali mambo mbalimbali kuhusu bajeti kuu ya serikali ya mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni pamoja na kuongeza kima cha chini cha mshahara ambacho hakikatwi kodi kutoka170,000 hadi 360,000 ili kumapa nafuu ya kodi mfanyakazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mwenyekiti kamati ya uchambuzi na ushauri ya chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania Poul Loisulie alisema ripoti ya kamati hiyo wamekwishaiwasilisha kwa Rais , Waziri mkuu pamoja na ofisi ya bunge.

Loisulie amesema serikali ikiongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 170000 hadi 360000 ambayo haikatwi kodi italeta nafuu kubwa katika kodi anayochangia mfanyakazi kwenye mshahara wake.

Serikali kupita wizara ya mambo ya ndani nchi irekebishe utararibu wa hati za kusafiria za muda mfupi badaya ya inavyofanyika kwa sasa.

Hata hivyo amesema katika mapendekezo hayo kamati imependekeza kutekeleza serikali ijikite kwenye kuhimiza viwanda vinavyotumia rasilimali  za ndani hasa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na uimarisha mkakati wa ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vilivyopo hasa vya kodi akisema lengo ni kuhakikisha kuwa uchumi unakua jumla jumla.

Kamati hiyo pia ilishauri kufufuliwa kwa vyanzo mfu vya mapatao, kutokana na kuwa havijawahi kuchangiwa kwa kiwango kinachotakiwa ikisema lengo ni kuongeza mapata ya serikali kwa manufaa ya wananchi.