Taarifa rasmi kutoka Simba SC zinaeleza kuwa leo jioni kikosi hicho kitaondoka kuelekea nchini Algeria kwa kupitia Dubai, UAE.
Mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura. utachezwa siku ya Jumamosi Machi 9, mwaka huu.
Simba SC watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kuwalaza JS Saoura Magoli 3-0 katika mchezo wao wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam.
Hadi sasa Simba SC wanashika nafasi ya pili kwenye kundi lao wakiwa wamejikusanyia pointi 6 kibindoni katika michezo minne waliocheza ambapo wamefungwa miwili na kushinda miwili ambapo walicheza nyumbani.