F Azam Fc - Tumedhamiria kupata alama tatu kwa Yanga | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Azam Fc - Tumedhamiria kupata alama tatu kwa Yanga


Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Ndanda Fc Mabingwa wa Afrika mashariki Azam fc wamepanga kumaliza hasira zao kwa vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga katika mchezo wao wa kiporo utakaopigwa April 29 mwaka huu katika dimba la uwanja wa Taifa.

Meneja wa Azam Philipo Alando amesema kuwa wamerejea Dar es salaam  tayari kwa maandalizi ya kuwavaa Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu kwani wamedhamiria kupata ushindi licha yakuwa wanawaheshimu Yanga SC.

"Ni mechi ngumu sana ukiangalia wao wamejipanga na sisi tumejiapanga sana kuhakikisha tuanshinda nechi hiyo ambayo itatoa taswira kwetu katika kuwania nafasi za juu katika msiamo huo" amesema Alando.

Aidha Alando ameweka wazi kuwa wamepokea kwa furaha taarifa za kutoka CAF juu ya Tanzania kuingiza timu nne katika mashindano ya kimataifa huku akizitaka timu zitakazo pata nafasi hiyo zisibweteke