Uongozi wa Baraza la Manispaa Mjini Zanzibar umesema kuwa utaendelea kushirikiana na viongozi wa manispaa ya Kinondoni ili kuweza kubadilishana mbinu bora katika sehemu zao za kazi.
Akizungumza Mkurugenzi wa manispaa ya mjini, Said Juma Ahmda amesema kuwa ujio huo wa viongozi wa manispaa ya kinondoni ni moja ya hatua ya maendeleo katika jamii.
CLP
Nae Meya wa Manispaa ya kinondoni jijini Dar Es Salam Benjamin Sita amesema kuwa wamekuja zanzibar kuja kubadilisha mawazo ya mambo mbali mbali kiwemo suala la mapato na kuimarisha undugu .
Pia amesema kuwa kitu kinachomvutia Zanzibar ni historia ni historia ya kitalii ya yenye kuvutia zaidi.
Hata hivyo Meya huyo amewataka viongozi wa manispaa ya mjini Zanzibar kuendeleza zaidi mashirikiano hayo ya dhati ili kuweza kuendelea siku hadi siku.