F Hakuna yoyote atakae vunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar-Abdulla Juma Mabodi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Hakuna yoyote atakae vunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar-Abdulla Juma Mabodi



NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi amewataka wanafunzi na jamii kuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuendelea kuimarisha Nyanja za kiuchumi na kijamii

Alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni tunu inayotakiwa kuenziwa kwa vitendo kutokana na kupelekea kuimarisha maendeleo ya nchi.

Rai hiyo aliitoa katika hafla ya kutoa vifaa vya shule ya Vijana wapenda maendeleo wa CCM.

“Hakuna mtu , kiongozi wa taasisi itakayo tokea kuvunja muungano huu ambapo kwa sasa umedumu zaidi ya miaka 55” alisema Dk Mabodi.
Alisema wakati umefika wa wananchi wa wilaya hiyo ya Kaskazini 'A' hasa sheria ya Kidoti na vitongoji vyake kupuuza maneno ya ulaghai yanayotolewa na vyama vya upinzani na badala yake kuthamini juhudi za kimaendeleo zinazotekelezwa na Serikali chini ya usimamizi wa CCM.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 alisema Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Mijini na vijijini ili wanufaike na Sera imara zinazosimamiwa na CCM.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi alifafanua kwamba maendeleo yaliyofikiwa nchini yametokama na misingi imara ya kiuongozi, kiitikadi na kimfumo iliyoasisiwa na waasisi wa Mapinduzi ya 1964,Muungano 1964 pamoja na waasisi wa TANU na ASP.

Katika hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wa shulei hiyo Dk. Mabodi aliesema CCM itatoa mabati ya kuezeka Kituo cha Afya cha Ndagoni pamoja na ujenzi wa choo, alichangia shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa matano ya shule hiyo, na vifaa mbali mbali vya kutumia mashuleni kwa wanafunzi watakaofaulu michipuo.