F Kiongozi wa upinzani 'awachana vikali' wanachama wake | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kiongozi wa upinzani 'awachana vikali' wanachama wake


Na Thabit hamaidu, Zanzibar

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Taifa, Hamad Rashid Mohammed amewataka wanachama wa chama hicho kufuata ilani yao kwa vitendo ili kupambana na vitendo viovu ikiwemo rushwa na wizi uliyomo katika jamii.

Ameyasema hayo huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar katika Ukumbi wa Madinat Al Bahri wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho.

Amesema msingi wa Mkutano huo unatokana na matakwa ya katiba ya ADC ambao ndio dira ya maendeleo ya wananchi katika kufikia malengo ya kuchagua viongozi ambao wanaweza na hatimae  kushika dola.

Aidha amesema kuwa mkutano huo utawezesha kutambua changamoto zinazowakabili wanachama
 Mwenyekiti huyo  amefahamisha kuwa umakini wa uongozi wa chama ndio msingi unaohitajika kwani ndio unaoleta maendeleo na kuweza kupata wanachama wapya ambao ndio watakaofikisha chama hicho kule wanakokuhitaji.

Akizungumzia suala la kisiasa amesema kuwa Duniani kote wanazingati a hali ya usalama na amani hivyo anazipongeza Serikali zote mbili kwa kudumisha  amani na utulivu uliopo  Nchini.

Pia amefafanua kuwa ADC ina uwezo wa kusimamia  hali ya usalama na amani na ndio mana imefanikiwa hadi leo kufikia Mkutano Mkuu wa chama Taifa na kuchagua Viongozi watakaoweza kusimamia na kuleta maendeleo.

Amesema kuwa suala la Bima ya Afya lazima lifanyiwe kazi ili kuwapunguzia wananchi gharama za matibabu sambamba na kufanikiSha afya bora kwa kila mwananchi.

Hata hivyo Hamad Rashid anaunga mkono Serikali suala la elimu bure hadi kufikia chuo kikuu lakini kwa upande wao wamsema kuwa  ni hatua kawa hatua hadi kufikia lengo hilo.