Kila chenye mwanzo mara nyingi huwa hakina mwisho sio maneno yangu ni maneno ya wahenga wenyewe. Wakati mwingine yawezekana uko kwenye mikono salama kwa huyo mpenzi wako ila naomba nikuibie siri kwamba ipo siku mtaachana tu kama utashindwa kufahamu namna sahihi ya kumfanya mwenza wako asikuache.
Hivyo kama ikitokea umeachana na mwenza wako haya ndiyo mambo ya msingi unayopaswa kuyafahamu ili kuondokana na msongo wa mawazo.
1. Usijaribu kumpigia simu
Hata kama ukimpigia simu haito saidia, sana sana utakua unajiumiza moyo kwa hisia unazozisababisha, na hii ndo nguzo kubwa ya kutumia ili undokane na mpasuko wa moyo, baada ya kuwa nae kwa kipindi kirefu namba yake ndo namba ulioipiga mara nyingi zaidi, kwa hio kwa vyovyote vile hisia zitakua zinakutuma kwa hali ya juu ili ufanye hivi, cha kufanya hakikisha umeifuta namba yake, na kama ukimpigia simu utajikuta unajiongezea miezi ya kutomsahau na kuumia kwa msongo wa mawazo, na mtoe kwenye orodha ya marafiki zako wa facebook, fikiri ukiwa facebook ukaona picha yake akiwa amekumbatiwa na mwanaume mwingine, nadhani unakiona kwanini mwanzo mpya ni muhimu.
2. Fanya mazoezi.
Bila mpenzi wako kukushika mkia, sasa hivi una muda wa kutosha kufanya mazoezi na kujiweka mwili katika hali nzuri, mazoezi ni mazuri kwa afya yako na ni njia nzuri ya kuondokana na hisia, ukiwa na mwili mzuri ni kitu kizuri cha kuvutia wasichana wapya.
3. Kaa mbali na marafiki zake pamoja na sehemu anazopendelea kushinda.
Kama unataka kuondokana na hisia zitokanazo na kukutana na mpenzi wako wa zamani kwa mda huu, inabidi ujitoe kwa baadhi ya mambo, inabidi ukate mawasiliano na baadhi ya marafiki ambao wapo upande wake na kuachana kabisa na baadhi ya sehemu mlizokua mnapendelea kwenda. Ni vitu vidogo kuvitoa kama utakuwa unahitaji pumziko la hisia, mawazo na akili yako kwa ujumla.
4. Tupa mbali kumbukumbu zozote zinazokukumbusha wewe na yeye.
Hilo doli, kadi na hayo maua aliyokupa kwa ajili ya siku yako ya kuzaliwa, hilo shati alilokununulia, hizo picha zilizotoka vizuri za yeye na wewe, ondoa zote na eiza uzitupe au uweke mbali, utavyoharakisha kutoa hivyo vitu ndo utakavyo sahau kwa haraka zaidi na kabla hujauliza "ndio", unaweza acha vitu ambavyo havikuletei hisia yeyote, ila nguo zake, vito vya kuvaa na vingine vyovyote vinavyo kukumbusha mbali viondoe.