F Rais Shein aongoza dua ya kumuombea Hayati Abeid Amani Karume | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Rais Shein aongoza dua ya kumuombea Hayati Abeid Amani Karume


Na Thabit Hamidu, Zanzibar.

Mamia ya wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla wamejitokeza katika Dua ya Pamoja ya kumuombea Rais wa awamu ya kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume iliyofanyika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi Visiwani humo.

Dua hiyo iliongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na viongozi wengine mbali mbali wa kitaifa.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa dua hiyo Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanna na Michezo ambae pia mtoto wa kiongozi huyo Balozi Ali Abeid Karume aliwataka viongozi nchini kuongoza kwa kuzingatia Maslahi ya wananchi kama kiongozi huyo wa kwanza wa Zanzibar.

Alisema baadhi ya viongozi huwa wanaongoza kwa kuzingatia maslah yao binafsi bila ya kuwajali wananchi wanawaongoza na kuenda kinyume na mtazamo na fikra za hayati karume.

“Katika siku hii ya kumbukumbu ya Mzee wetu huyu kitu cha msingi cha kijifunza ni kuongoza kwa kuzingatia maslahi ya wananchi tunaowaongoza na si kuongoza kwa kujijali wenyewe”alisema.

Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira January Yusuf Makamba alisema kupitia miaka 47 tokea kuwawa kwa kiongozi huyo kitu cha msingi ambacho serikali imekuwa ikimuenzi kwa vitendo ni kuimarisha Muungano wa Tanzania.

“licha kufanya dua hii ila serikali ya jamuhuri imekuwa ikimuenzi kwa vitendo kwa muungano aliotuachia mzee wetu karume na baba wa Tiafa Jurias Nyerere”alisema Januari Makamba.

“laiti angekuwa hai angefurahia jinsi muungano huu ulivyoimarika wa Nchi zetu” alisema Januari Makamba.

Aidha aliwataka Viongozi na Vijana nchini kujifunza Mambo mbali mbali kupitia maisha ya Mzee karume, Katika Dua hiyo viongozi wa kuu wa Nchi na wastaafu waliohudhuria wamepata fursa ya kumuombea dua hapo na kuweka mashada ya maua.