Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa Bunge analoliongoza si dhaifu hata kidogo. Amebanisha hayo leo Bungeni wakati mkutano wa 15 wa Bunge ulianza jana ukiendelea.
Utakumbuka hapo jana Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.
"Bunge hili si dhaifu na kama mtu yeyote atajaribu kuingia kwenye 18 zetu anaalikwa kwenye mchezo huu," amesema Spika Ndugai.
Hatua ya kutofanya kazi na CAG ilifikia baada ya kauli yake ya 'udhaifu wa Bunge' aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Hivyo Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kubaini kuwa lugha aliyoitumia ililenga kulidharau Bunge na kushusha heshima ya chombo hicho cha Dola, hivyo kamati hiyo ilimtia hatiani.