F TMA yatoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

TMA yatoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), yatoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi, zitakazoacha athari katika shughuli ikiwepo baadhi ya makazi kuzingirwa na maji.

Meneja wa Kituo Kikuu cha Utabiri wa TMA, Samwel Mbuya amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujiandaa kwani kutakuwa na mawimbi makali, upepo mkali na mvua kubwa.

Mikoa iliyotajwa kukumbwa na hali hiyo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Amesema kutakuwa na kutawanyishwa/kupeperushwa kwa takataka mitaani, kuanguka kwa majani na matawi madogomadogo ya miti, kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafiri baharini pamoja na ugumu wa upatikanaji wa samaki.