F Wajenga visima 100 vya maji kuwasaidia wanafunzi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wajenga visima 100 vya maji kuwasaidia wanafunzi


Shirika lisilokuwa la kiserikali la African Reflection Foundation limejenga visima 100 katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ambavyo vimesaidia kupunguza adha ya maji kwa wananchi na wanafunzi kwenye maeneo ya Shule.

Balozi Mdogo wa Visiwa vya Shelisheli ambaye ndiye mtekelezaji mkubwa wa miradi hiyo Maryvonne Pool amesema wakati wa uzinduzi wa kisima kipya kilichojengwa kwenye Shule ya msingi Mikere wilayani Mkuranga kuwa aliamua kuanza kujenga visima baada ya kuona adha walizokuwa wakipata wananchi kwa kukosa maji safi na Salama.