Na Rahel Nyabali, Tabora.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Upuge WilayaniUyui Mkoani Tabora wameiomba serikali kukifufua kituo cha kilimo na ujenzi kilichopo kijijini hapo kilichokua kinatoa mafunzo ya wafanyakazi, kutengeneza vipuli na zana za kilimo na ufundi seremala.
Wakizungumza kituoni hapo wamesema kuwa kituo hicho kina mchango mkubwa katika malengo ya serikali ya kuwa na nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda.
Mashaka Salum mkazi wa kijiji cha Upuge wilayani humo amesema vifaa vya kituo hicho bado vipo walivyokuwa wanatumia kujifunza kuchonga vipuli na zana za kilimo, mafunzo ya wanyama kazi ambapo kusimama kwa kituo hicho kimesababisha vananchi kukosa elimu iliyokuwa inatolewa kituoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Gift Msuya amesema kituo hicho chenye eneo lenye ukubwa wa ekari 220 kinaweza kuwa kitovu cha uchumi wa wilaya hiyo endapo kitatumika ipasavyo katika uwekezaji wa kilimo.
“Nimemuomba mkurungezi mtendaji wa Halmashauri amwandikie barua katibu mkuu wa wizara ya kilimo ili kama inawezekana hiki kituo kiwe chini ya umiliki wa halimashsuri ya wilaya’’ amesema Mkuu huyo wa Wilaya. .