Na Rahel Nyabali, Tabora
Ili kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama nchini wadau binafsi Mkoani Tabora wametakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuchangia ujenzi wa Nyumba za Askari Polisi ziweze kukamilika katika ubora unaotakiwa, hatua ambayo itasaidia kuvutia wawekezaji mbalimbali kuwekeza nchini.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ambaye amekuwa mgeni Rasmi katika harambee iliyowakutanisha wadau wa maenedeleo wilayani Tabora mkoni Tabora amesema lengo ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuchangia nyumba za Askari polisi.
“Tukijipanga vizuri hapa tuna jeshi la polisi, jeshi la Magereza, tunavijana wazuri wa jeshi la wananchi JWZ, bodaboda tukiamua kujenga kwa umoja tutatoka hapa tulipo” Amesema Mwanri.
Aidha ametoa rai katika matumizi ya fedha hizo zitakazo tumika katika ujenzi kufanya kazi husika ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa viwango stahiki.
“Hela hii haita liwa hawa watu ndio wanaosukuma ndani wakitumia fedha hii kinyume na ujenzi wa nyumba hizi watasukumwa ndani wao” amesema Mwanri.