Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Joseph Salun (28) mkazi wa kijiji cha Mwakwaru ngalitati katika wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro amefukua kaburi la Baba yake mzazi aliyezikwa miaka mitatu iliyopita na kisha kutoa mabaki ya mwili wa marehemu huyo nje ya kaburi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu marehemu zimeelea kuwa sababu Kijana huyo Joseph alieleza kuwa amefukua kaburi hilo kwa lengo la kuchukua Blanketi lilozikwa nalo marehemu kwa ajili ya kujisitiri wakati huu wa hali ya baridi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Hamisi Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambali amesema ni la kushngaza.
"Kijana ameamua kufukua kaburi la baba yake bila kibali, na baba yake alikuwa ameshazikwa miaka mitatu iliyopita kisa kilichomfanya afukue alikuwa na madai kwamba kutokana na hii hali ya hewa yeye alikuwa anahitaji Blanketi alilokuwa amezikiwa baba yake," amesema Kamanda wa Polisi.