Wafanyabiashara wa samaki katika soko la Sabasaba wamelalamikia tatizo la kukosekana kwa samaki kwa kipindi cha mwezi mmoja kwasababu ya upepo mkali kwenye Ziwa Tanganyika jambo lililochangia uhaba wa samaki na hivyo kupanda bei kwa kiwango cha juu.
Baadhi ya wavuvi wamesema kwa sasa wanaoweza kuvua ni wachache na wamekuwa wakipandisha bei ya samaki kwa kiwango hicho cha juu na hivyo kuleta usumbufu kwa walaji.
Kwa sasa samaki mmoja mkubwa aina ya Kuhe na Kichanga wanaopatikana katika ziwa hilo lililoko umbali wa kilomita 112 kutoka Sumbawanga mjini anaweza kuuzwa hadi shilingi 60,000 na wa saizi ya kati shilingi 30,000 - 45,000.