F Fahamu ugonjwa wa kuvimba macho kwa kuku na jinsi ya kutibu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Fahamu ugonjwa wa kuvimba macho kwa kuku na jinsi ya kutibu


Ugonjwa wa kuvimba macho kwa kuku ni miongoni mwa magonjwa ambayo chanzo chake mara nyingi hutokana na mfumo wa hewa. Haya ni magonjwa ambayo ni sugu na huwaathiri kuku kwa kiwango kikubwa sana.

Sasa tuone chanzo cha ugonjwa huu wa kuvimba macho
Maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na kwenye vimelea
Kupitia mfumo wa hewa kutoka kuku wagonjwa
Kupitia mayai, hivyo maambukizi huendelea kutoka kizazi hadi kizazi

Dalili za ugonjwa huu ni;
Kuku kukoroma
Kuku hutoa makamasi
Kuku wanakohoa kwa muda mrefu, wiki hadi mwezi
Kuvimba macho
Kutingisha kichwa
Vivo vya kuku viaweza kufikia hadi asilimia 20 Uchunguzi
Kamasi nzito zenye usaha zilizotapakaa kwenye pia, koromeo, mapafu na vifuko vya hewa

Jinsi ya kutibu ugonjwa huu.

Madawa aina ya sulfa na antibiotiki
Kwa ushauri zaidi  waone watalamu wa vifugo ili wakupe maelekezo kamili