Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Dkt. Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa hawajaenda nyumbani kwa Mengi kumsifia ila wameenda kutoa pole kwa familia.
Mzee Mwinyi ameyasema hayo leo, alipofika kutoa pole kwa familia ya Mzee Mengi, ambapo pamoja na hayo amesema kuwa Dk. Mengi kwa muda wote aliokaa duniani alikuwa akigawana na Watanzania wenzake alichonacho.
"Hatujaja kumsifu Mengi ila tumekuja kutoa pole kwa familia, kuondoka kwake ni pigo kwangu na kwa familia yake na watu wote, mtu huyu alikuwa mkarimu si mkarimu wa mali tu ni mkarimu wa Fikra wa mawaidha," amesema Mzee Mwinyi.
"Bwana huyu kwa muda wote amekaa duniania alikuwa akigawana na Watanzania wenzake kwa kile alichokuwa nacho, leo Mzee Mengi ametutoka, natoa pole kwa watoto wake, ndugu zake, jamaa zake," amesema Mzee Mwinyi."