F Mwanasiasa wa Upinzani aitaka ICC imlipe fidia ya Euro Milioni 68 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwanasiasa wa Upinzani aitaka ICC imlipe fidia ya Euro Milioni 68


Mwanasiasa wa Upinzani nchini DR Congo, Jean-Pierre Bemba ameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kumlipa zaidi ya euro milioni 68 kama fidia kutokana na kufungwa gerezani bila kuwa na hatia .

Makamu huyo wa Rais wa zamani wa DR Congo alituhumiwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita uliotekelezwa nchini humo Kati mwaka 2002 na 2003 lakini aliachiliwa huru mwezi Juni 2018 baada ya kumaliza miaka 10 jela .

Baada ya kukamatwa kwake, Mahakama hiyo ilikamata mali zake, ikiwa ni pamoja na zile za nchini Ureno, Ubelgiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

Aidha Bwana Bemba amesema kuwa kati ya fedha hizo anazotaka alipwe fidia euro milioni 26 ni fidia ya kukaa miaka yote Gerezani bila hatia kutokana na kutafsiri sheria vibaya huku euro 42 ikiwa ni fidia kutokana na uharibifu wa mali zake madai ambayo Ofisi ya mashitaka ya ICC inayapinga .