Ni rasmi timu za African Lyon ya Dar es Salaam na Kagera Sugar ya Kagera zimeshuka daraja kutoka Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na msimu ujao zitacheza Ligi Daraja la Kwanza.
Mwadui FC na Stand United za Shinyanga zitacheza mechi za mtoano dhidi ya timu za Geita Gold FC na Pamba SC kuamua kubaki au kuondoka kwenye ligi kuu.
African Lyon imemaliza ligi ikiwa mkiani na pointi 23 huku Kagera Sugar ikiwa na pointi 44, sawa na Stand United na Mwadui wakitofautiana kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku matokeo baina ya Kagera Sugar na Stand mara mbili walizokutana (Head-to-Head) pia yakichangia anguko hilo la Kagera Sugar
Mwadui itacheza mtoano na Geita Gold ya Daraja la Kwanza huku Stand ikitarajiwa kucheza na Pamba kuwania kubaki ligi kuu, wakati wapinzani wao wakiwaniA kupanda daraja.