F Picha: Rais Magufuli katika msiba wa rafiki yake aliyesoma naye shule ya msingi Chato | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Picha: Rais Magufuli katika msiba wa rafiki yake aliyesoma naye shule ya msingi Chato


Rais Dkt. John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Festo Rutamigwa Isokoza alipoongoza waombolezaji kuaaga mwili huo katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya
Lugalo jijini Dar leo.

Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo alifanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile JKT Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha.

Alikuwa rafiki mkubwa wa  Rais Dkt Magufuli ambaye  walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita  na baadaye elimu ya sekondary katika Seminari ya Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.