F TANZIA: Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi Afariki Dunia | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

TANZIA: Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi Afariki Dunia


Waziri wa zamani Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi, amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu, Katibu wa NEC – Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey PolePole ametangaza.

Marehemu aliwahi kuwa Mbunge wa Mlalo, Huko Lushoto, Waziri wa TAMISEMI na Mwenyekiti wa Kamati moja ya Bunge. Endeelea kuwa karibu na Muungwana Blog kwa taarifa zaidi.