F Faida za kutumia ukwaju kiafya | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Faida za kutumia ukwaju kiafya


Zifuatazo ndizo faida za ukwaju ambazo zitakushawishi siku nyingine kuagiza glasi ya juisi ya ukwaju, na kama ni 'waziri wa mambo ya ndani' ya nyumba, au una fahamiana na 'waziri husika' basi agiza aendapo gulioni asiache kuchukua fungu la ukwaju wa kutosha walao wa wiki kama si mwezi mzima.

Faida 10 za ukwaju:
1. Chanzo kizuri cha viua sumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)

2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"

3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo

4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni

5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa

6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)

7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)

8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo

9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda

10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo