F Kongamano la ujasiriamali kwa wanawake na vijana ni fursa - DC Hanang | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kongamano la ujasiriamali kwa wanawake na vijana ni fursa - DC Hanang


Na John Walter-Katesh-Hanang

Kuelekea katika Kongamano la ujasiriamali Wanawake na Vijana mkoa wa Manyara chini ya Mbunge wa Viti maalum (CCM),  Ester Mahawe linalotarajiwa kufunguliwa jumamosi ya wiki hii Katesh mjini wilaya ya Hanang, Mkuu wa wilaya hiyo amesema wilaya yake itaongoza Kimkoa.

Kongamano hilo ambalo litafungwa Julai 20 na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama katika mji wa Babati, litalokwenda sambamba na kusaka vipaji vya waimb,aji wa muziki wa aina zote ambapo kwa mujibu wa Mheshimiwa Mbunge Ester Mahawe mshindi wa kwanza atajinyakulia shilingi Milioni moja na nusu.

Mkuu wa wilaya ya Hanang, Joseph Mkirikiti ameiambia Muungwana Blog kuwa kutokana na wilaya hiyo kuwa na vijana wengi wenye vipaji  anaamini itakuwa ni fursa kwao kuwa washindi.

Amesema kongamano hilo ni fursa kwa vikundi mbalimbali vya  wajasiriamali,wawekezaji wadogo ambao watapata nafasi ya kuwaona wataalamu mbalimbali  watakaohudhuria kuapata uzoefu mpya kibiashara.

Mbali na hayo, DC Mkirikiti amesema wilaya yake ina Fursa za Utalii kupitia Mlima Hanang, kilimo,Mifugo, pamoja na madini ambayo yametoa ajira kwa wengi.