Mahitaji
- Pumba ya mahindi sadolini 1.
- Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
- Dagaa sadolini 1.
- Kilo moja ya soya.
- Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.
Namna ya kuandaa
- Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
- Saga hadi zilainike.
- Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
- Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
- Anika kwenye jua la wastani.
- Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
- Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.