F CT Scan ya Hospital ya Benjamini Mkapa yahudumia wagonjwa zaidi ya 2000 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

CT Scan ya Hospital ya Benjamini Mkapa yahudumia wagonjwa zaidi ya 2000



Na.Enpck Magali,Dodoma

Mkuu wa Idara ya Radiolojia katika Hospital ya Benjemini Mkapa iliyopo Jijini Dodoma  Henry Mwansasu,amesema idadi ya wagonjwa wanao patiwa huduma kwa kutumia kipimo cha kuchunguza tishu na ogani za mwili kwa kutumia mionzi (CT SCAN) wanafikia zaidi ya 2000 kwa kipindi cha miezi sita.

Mwansasu ameyasema hayo July 03 mwaka huu Hospital hapo wakati wa mazungumzo maalamu na Blog hii na kuongeza kuwa,Mashine ya CT Scan iliyopo Hospitalini hapo ni ya kisasa na ilianza kutumika rasmi July 2017 na kuwa ina uwezo wa kutoa picha bora na  za kutosheleza.

"Unapompima mgonjwa,uwezo wa CT Scan kwamba hii ni ya kisasa inatafasiriwa na ubora na kiasi cha kutosha cha picha,hii ya kwetu inatoa picha zenye ubora wa kimataifa,sio kama za huko mtaani ambazo hazina ubora"Alisema Mwansasu.

Mwansasu ameongeza kuwa,kutokana na huduma wanayoitoa wamekuwa wakipokea wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali nchini ambapo hupatiwa matibabu ya kibingwa klingana na matatizo yanayowasumbua.

"Wastani kwa siku wanahudumiwa wagonjwa kumi hadi inshirini wa CT Scan,ambapo kwa miezi sita (yaani kuanzia mwezi January hadi June 2019) wanafikia  idadi ya wagonjwa  2300 hadi 2500,hii yote ni kutokana na kwamba huduma zetu zina ubora wa hali ya juu,kwani hata ikilazimika hayo matibabu yakafanyike Muhimbili au nje ya nchi,yale majibu yanakuwa yamekidhi vile viwango kwa hiyo mgonjwa anaendelea na matibabu badala ya kupimwa upya"Aliongeza Mwansasu.

Na kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Uhusiano  na Mawasiliano wa Hospital hiyo Kareem Meshack yeye amesema kuwa wameweka utaratibu maalaumu wa kuwahudumia wagonjwa ili kuhakikisha kuwa hakuna usumbufu wala malalmiko yasiyo ya lazima.

"Huduma bora ni haki ya kila mgonjwa sio jambo la kuomba,na ndio maana tumeweka namba zetu za simu katika kila kona ya Hospital yetu hivyo mgonjwa akipata changamoto yeyete ile atapiga namba hizo,wagonjwa katika hospital hii hana sababu ya kutoka hapa akiwa maekwazika kwani wahudumu wetu wapo kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma iliyo bora"